advertise with us

ADVERTISE HERE

MJUKUU WA MZEE AKILIMALI "LAVALAVA FEKI" ASEMA ZESCO HAWACHOKOKI KWA MKAPA

Shabiki kindaki wa Dar Young African (Yanga) amejigamba kwamba Zesco hawezi chomoka uwanja wa taifa kwani Yanga ya sasa si ile ya mwaka jana.

Shabiki huyo mwenye kelele nyingi mitaani amesikika akisema hata Simba waujaze uwanja kuishabikia Zesco bado watashinda tu mchezo huyo. Jamaa huyo aishie maeneo ya kimara amekuwa akijifananisha na msanii wa WCB Lavalava na ni shabiki mkongwe  wa klabu ya Yanga.

Jamaa huyo inasemekana ni mjukuu wa mzee Akilimali (mwenyekiti baraza la wazee Yanga) na  amekuwa akiitabilia Yanga kwa muda mrefu na amesema hata mchezo huu alizungumza na babu yake na kuambiwa ni lazima washinde.
            Lavalava feki wa tatu kulia akishangilia kwenye moja ya mechi ya taifa staz

Shabiki huyo amekuwa akisafiri mara nyingi na timu hiyo kuelekea mikoani ambapo hivi majuzi alipatikana jijini mwanza wakati Yanga ikijiandaa na mchezo dhidi ya Zesco.
Uongozi wa Amospoti.com unamtafuta kwa udi na uvumba uweze kumkabidhi jezi mpya ya Yanga shabiki huyo endapo timu hiyo itafanya vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya Zesco United.

Post a Comment

0 Comments