advertise with us

ADVERTISE HERE

MESSI KUTIMKA BARCELONA BURE MWAKA 2020/21

Uongozi wa Barcelona umekaa kimya juu ya hatma ya staa huyo kusalia Nou camp mpaka mwaka 2021.

Mchezaji huyo mwenye miaka 32 ana mkataba unaomalizika mwaka 2021 lakini anauwezo wa kuondoka mchezaji kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu wa 2019/2020.  Uongozi wa Barcelona ulisaini mkataba wa mwisho na mchezaji huyo mwaka 2017 na unaamini Messi hatasita kuongeza mkataba mwingine klabuni hapo baada ya huu alionao kumalizika mwaka 2021. 

Taarifa za ndani za Barcelona zinaamini Messi ataondoka kama mchezaji huru na kujiunga na vilabu vingine kama walivyofanya baadhi ya  wachezaji maarufu na muhimu klabuni hapo akiwemo Xavi Hernandez na Andre Iniesta.

Raisi wa Barcelona bwana Bartomeu alinukuliwa akisema " Tumesaini na Lionel Messi mkataba miaka miwili iliyopita na mkataba wake unamalizika baada ya miaka minne ambapo ni msimu wa 2021, lakini pia mkataba huo unamruhusu mchezaji huyo kuondoka Barcelona,kustaafu au kuendelea na Barcelona. Iniesta ,Puyol na Xavi walikuwa na mikataba ya namna hii na hatuna wasiwasi na hatma ya Lionel Messi. Tunaamini ataendelea kuwepo hapa hata baada ya 2021 maana amejiwekea heshima kubwa ndani ya klabu hii."

Messi aliumia mazoezini kipindi cha matayarisho na amekosekana baadhi ya mechi huku Barcelona ikiambulia pointi 4 tu katika michezo mitatu ya ligi.

Post a Comment

0 Comments