advertise with us

ADVERTISE HERE

KOCHA SIMBA AIPA MBINU ZA USHINDI YANGA,AZAM

PATRICK Aussems, Kocha pekee Bongo raia wa Ubelgiji amesema kuwa Yanga na Azam FC zinatakiwa kuutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo kwenye michezo ya kimataifa kabla ya kwenda ugenini ambako huko kuna shida kubwa.

Msimu uliopita Simba ilitinga hatua ya robo fainali michuano ya kimataifa kwa kushinda mechi zake zote za nyumbani kabla ya kutolewa na TP Mazembe baada ya kulazimisha sare kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.

 Aussems amesema kuwa anatambua kwamba Yanga na Azam FC zina kazi kimataifa wanachotakiwa kufanya ni kutumia vema uwanja wa nyumbani.

“Unajua michuano ya kimataifa nimeona namna ushindani wake ulivyo kila timu inapambana kupata matokeo nyumbani kwa kuwa kuna nguvu ya mashabiki na hakuna presha kubwa hicho ndicho ninachoamini kitafanyika kwa wawakilishi waliopo kimataifa.

“Muda wa kufuatilia kwa kweli wenzangu wanafanya nini sina kutokana na kazi yangu ndani ya Simba ila ninaamini inawezekana kwao wote Azam na Yanga kushinda,” amesema. 

Post a Comment

0 Comments