advertise with us

ADVERTISE HERE

KIONGOZI YANGA AANZA KUTOA VISINGIZIO VYA KUFUNGWA DHIDI YA ZESCO

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ameibuka na kusema kukosekana kwa kiungo Mapinduzi Balama katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika leo dhidi ya Zesco United inaweza kuwa pengo kwa timu hiyo.


Mkwasa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ndani ya klabu ya Yanga, ameeleza kuna uwezekano kukawa na udhaifu eneo la kiungo ambalo Balama aling'ara vema kwenye mechi ya kwanza.

Mkwasa amefunguka kuwa Balama alikuwa silaha muhimu katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam dhidi ya Zesco, haswa kutokana na kazi nzuri ya kumpa wakati mgumu kwa kumdhibiti vizuri straika wao Jesse Were.

"Ni kweli kukosekana kwa Balama kunaweza kukawa na pengo kwa namna moja ama nyingine sababu tuliona alichokifanya katika mechi ya kwanza.

"Ni mchezaji ambaye anaweza kucheza vizuri eneo la katikati na alifanya kazi kubwa ya kupambana na mikikimikiki ya washambuliaji wa Zesco ikiwemo Jesse Were ambaye alimpa wakati mgumu.

"Naamini Kocha Mwinyi Zahera anajua nini cha kufanya na atatafuta namna nyingine ya kuziba pengo kwasababu ni majukumu yake ya kazi ambayo siwezi kuyaingilia," alisema Mkwasa.

Aidha, kwa upande mwingine Mkwasa amewaasa wachezaji wa Yanga kuhakikisha wanaingia uwanjani bila kuvunjika moyo sababu ya matokeo waliyoyapata katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bali waingie wakijiamini kwa ajili ya kuipambania timu ili iweze kushinda na iweze itinge hatua ya makundi.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza Yanga ilienda sare ya 1-1 na miamba hao wa Zambia ambapo leo wanahitajika kushinda mechi itakayopigwa kunako dimba la Levy Mwanawasa ili kuendelea kusalia kwenye mashindano na kuwaondoa Zesco.

Post a Comment

0 Comments