advertise with us

ADVERTISE HERE

SIMBA WAWATIA MOYO YANGA

Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kocha wa zamani wa Simba na Dodoma FC, amesema kuwa bado nafasi ya Yanga kushinda mbele ya Zesco ipo endapo wachezaji watashusha presha waliyonayo na kuacha kupaniki.

Yanga juzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Zesco ya Zambia kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika na wanatarajia kurudiana nao Septemba 27.

Julio alisema kuwa kwa sasa wachezaji wa Yanga baada ya kupata sare, hawapaswi kupaniki bali washushe presha ili kuwa katika ubora wao.

“Mpira una matokeo ya kikatili, kupata sare wao siyo wa kwanza na wanaweza kupindua meza kibabe endapo watatulia na kushusha presha ambazo wanazo kwa sasa.

“Makosa madogomadogo ambayo wameyaonyesha ni muda wa kuyafanyia kazi na ninaamini watafanya makubwa na kuushangaza ulimwengu, nafasi bado wanayo,” alisema Julio.

Post a Comment

0 Comments