BETI NASI UTAJIRIKE

RONALDO,ICARDI NA SALAH WAPIGA GOLI 12 WIKIENDI HII

Wikiendi hii imeleta mshangao kwenye soka baada ya vinara wa ufungaji kuonyesha uwezo wa juu katika ligi zao
 1. Salah 
Ndie kinara wa ufungaji ligi kuuEngland msimu huu akifunga jumla ya magoli 28 akiwaacha mpinzani wake  Harry Kane kwa jumla ya mabao 4. Salah alisajiliwa kutoka AS ROMA na ameweza kuhimili ligi kuu England kwa kipindi kifupi na kufanya vizuri.
siku ya jumamosi ya tarehe 17 Salah aliifunga Watford magoli manne na kumfanya aweke rekodi mpya ya ufungaji. baadhi ya wachambuzi wameanza mlinganisha na wachezaji mahili kama Cristiano Ronaldo na lionel Messi kitu ambacho si kweli.

2. ICARDI
Mwanzoni mwa msimu wa 2017/18 Icardi aliuanza vizuri sana kwa kufunga mara lwa mara na kumfanya kuwaniwa na timu kadhaa kipidi cha usajili wa dirisha dogo. Baada ya tetesi nyingi kuzagaa na yeye  kushindwa kuhama Inter milan hakufanya vizuri baadhi ya mechi na baadhi ya viongozi kumhusisha na kutaka kuihujumu timu. mechi dhidi ya timu yake zamani  Sampdoria amedhihirisha kurudi kwenye kiwango cha hali ya juu baada ya kuifunga goli nne na kuweka rekodi ya kufikia magoli 100 kwenye mechi 180 alizocheza Serie A na kushika nafasi ya pili kwenye ufungaji akiwa na magoli 18.


3. C.RONALDO
Anazidi imalika siku hadi siku kwa kuvunja rekodi zake mwenyewe. msimu huu hakuanza vizuri na alizidiwa kwa kiasi kikubwa  na mpinzani wake Lionel Messi kwa wingi wa magoli la liga. Ronaldo mwenye miaka 33 amerudi uwanjani kwa kasi na kuushangaza ulimwengu baada ya kufunga magoli 4 dhidi ya Girona na kupanda nafasi ya 2 kuwania kiatu cha dhahabu. mwanzoni mwa msimu Ronaldo alinikuliwa akiwaambia wachezaji wenzake  kuwa atamaliza namba moja ufungaji La Liga kutu ambacho wachambuzi wengi walikipinga kutokana na yeye kutocheza mechi 5 za mwanzo na hata aliporejea uwanjani alionekana kufanya vibaya sana. kwa sasa anajumla ya magoli 22 la liga akiachwa na mpinzani wake Lionel Messi kwa magoli 3

Post a Comment

0 Comments