Piers Morgan mshabiki maarufu wa Arsenal kupitia mtandao wa Twitter aliandika "hakuna mchezaji bora zaidi ya Mohammed Salah tangu astaafu Thiery Henry"
Kupitia mtandao huo Beki mstaafu wa Manchester United alimjibu Mo Salah ni mwenye kiwango kizuri msimu huu ila hawezi ingia hata top ten ya wachezaji waliofanaya vizuri mara baada ya Thiery Henry kuondoka Arsenal. Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 14 bora zaidi ya Mo salah .
Cristiano Ronaldo, Drogba,De Gea, Hazard, De Bruyne, Suarez, Yaya, Aguero, Kompany, Van Persie, Costa ,Kane,Tevez,Silva.
Morgan aliendelea kumchokonoa Garry Neville kwa kumwambia " Huna ujuzi wa kutambua wachezaji bora ila mimi naweza kuelezea nini kilitokea Valencia" Garry Neville alimjibu kwa kicheko
Salah alijiunga na Liverpool mwaka 2017 na ameisaidia timu hiyo kwa kiasi kikubwa katika michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi kuu kwa kufunga magoli 31 . Mchezaji huyo amezidi kuwa kinara msimu huu kwa kasi na umakini wa kufunga magoli.Mo Salah ana magoli 23 nyuma ya Harry Kane mwenye magoli 24 katika ligi.
Je Mo Salah anaweza maliza kinara wa Ufungaji Ligi kuu Uingereza?
0 Comments