Usiku wa tarehe 31 mwezi Januari umekuwa mchungu kwa vilabu vikubwa vya Uingereza baada ya kushindwa kutamba.
Eriksen akishangilia bao la kuongoza
TOTTENHAM 2-0 MANCHESTER UNITED
Ndani ya sekunde 11 ya mchezo kuanza Erikson aliwanyamazisha mashabiki wa machester united kwa kumalizia pasi ndefu toka kwa Harry Kane.
Dakika ya 28 beki wa Manchester United Phil Jones alikamilisha ushindi kwa kujifunga mwenyewe. Matokeo hayo yanaifanya United kuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi 15.
CHELSEA 0- 3 BOURNEMOUTH
Ni timu iliyopanda daraja msimu huu na imekuwa ikifanya vizuri zaidi hasa inapokutana na timu kubwa. mzunguko wa kwanza wa ligi ilifungwa na Manchester city pekee kwa timu zilizo nafasi za juu. mzunguko wa pili imeanza vyema kwa kumfunga Chelsea 3-0 darajani. Matokeo hayo yanaipeleka Chelsea nafasi ya 4 katika ligi ikizidiwa magoli ya kufunga na Liverpool.
MANCHESTER CITY 3-0 WESTBROMWICH
Ushindi dhidi ya Everton unamfanya Manchester City amwache mpinzani wake Manchester United kwa pointi 15. Fernandinhoalifungua milango ya kufunga Kelvin De Bruyne akapachika bao la pili na Sergio Aguero akakamilisha bao la tatu. msimu huu Manchester city imefungwa mchezo mmoja pekee dhidi ya Liverpool.
matokeo mengini ni
Everton 2-1 Leicester city
New Castle 1- 1 Burnley
Southhampton 0-0 Brighton
Stoke city 0- 0 Watford
0 Comments