advertise with us

ADVERTISE HERE

WENGER KUINGIA IKULU KWA MARA YA KWANZA

Kocha wa Arsenal  Arsene Wenger ni mmoja wa wageni muhimu waliokaribishwa na rais mpya wa Liberia katika hafla ya kuapishwa kwake
 Mwaka 1988-1992 Arsenal akiwa kocha wa Monaco , George weah alikuwa ni moja wa wachezaji kipenzi wa Wenger. mwaka 1995 Weah alishinda tuzo ya Ballorn D'OR na ndiye mwafrika pekee kufanya hivyo.
Weah alichaguliwa kuwa Rais wa Liberia mwishoni mwa mwaka 2017 kwa asilimia 62.5 dhidi ya mpinzani wake na ataapishwa januari 22.
Kuna tetesi Wenger akashiriki  uapishwaji huo kutokana na kufungiwa mechi nne za ligi. uapishwaji wa Weah utakuwa ni tarehe 22 , Arsenal itacheza tarehe 20 na crystal pallace pamoja na mchezo wa nusu fainali tarehe  24 dhidi  ya chelsea kombe la Carabao.
 Wenger kuhusu Weah
"Ukitazama maisha ya Weah ni kama filamu nzuri yenye kushangaza na kutokuwezekana. nilikutana nae Monaco alionekana hamjui mtu yeyote, na hafanani kama mchezaji wa mpira. mwaka 1995 alikuwa mchezaji bora wa dunia na sasa ni rais wa Liberia. alikuwa na mipango katika safari yake.
Alipokuwa anaiochezea Monaco ni kipindi ambacho nchi yake ilikuwa katika vita na niliona jinsi alivyokuwa anapata shida.
Alikuwa na Upendo kwa nchi yake na  watu wake, kuwajali na kuwatunza. nakumbuka jinsi alivyokuwa analia wakati wa vita nchini kwake.
Hii ni stori nzuri sana na namtakia uongozi mwema"

Post a Comment

0 Comments