advertise with us

ADVERTISE HERE

MOURINHO: SANCHEZ ATAWAKABILI TOTTENHAM SPURS

Kocha wa Manchester United amethibitisha kuwa Alexis Sanchez atakuwepo katika mchezo dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Mourinho alisema Manchester United ni mahali panapompa furaha , baada ya kudroo katika michezo mitatu ya mwezi December na kuachwa wingi wa pointi na mahasimu wao Manchester City, Kocha huyo amefurahishwa na mwenendo wa timu hiyo kwa mwezi januari baada ya kushinda michezo 5 mfululizo.

Alexis Sanchez anategemewa kuanza tena  katika mchezo wa FA dhidi ya  Spurs baada ya ule wa ijumaa iliyopita.
Mourinho aliiambia MUTV kwamba " tumeshinda michezo mitano mwezi Januari , michezo mitatu ya ligi na miwili ya vikombe hiyo ni dalili tosha kwamba tuka makini, Tunajitahidi kuibalansi timu , ila kuto ruhusu kufungwa ni ngumu mno kwa ubora wa ligi hii, lengo letu ni kufunga magoli na kushinda mechi , tunahitaji pointi na tunafanikiwa kutokana na ubora wa timu yetu.
Spurs wapo nyuma ya Tottenham kwa pointi 8 na wanahangaika kutafuta nafasi ya nne. hilo halimtishi mourinho na anaamini atashinda katika mchezo huo.

"Spurs ni moja ya timu nzuri katika ligi yetu, si kwa kufuata makombe kwani wapo mbali sana na wanatafuta nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa ulaya . wanaweza fikia levo hiyo kwa kuwa wana wachezaji wazuri, kocha mzuri na wanajituma sana " alisema Mourinho.

Post a Comment

0 Comments