BETI NASI UTAJIRIKE

MASHABIKI ARSENAL WAMTAKA CECH KUSTAAFU

Kipa wa Arsenal amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuruhusu kufungwa na Swansea 
 Mashabiki wa Arsenal walionekana wenye hasira baada ya mchezo huo kumalizeka kwa Swansea kushinda 3-1 .  Mchezo huo ulianza kwa kasi na Arsenal walipata bao la kuongoza katika dakika ya 32 kabla ya Swansea kusawazisha katika dakika ya 34. kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 61 Mustafi alimrudishia mpira kipa Cech ambaye alikosea kuupiga na ukamkuta   mshambuliaji wa Swansea Jordan Ayew  aliemalizia golini.
 Cech akijaribu kuupiga mpira aliopigiwa na Mustafi.
Jirdan Ayew akishangilia bao la pili lililosababishwa na uzembe wa Cech.
Kupitia mtandao wa Twitter Petre Cech aliandika " Makosa hutokea na ni sehemu ya mchezo, nimekuwa nikijiamini kwa asilimia 100sifurahishwi na sikutegemea hili kutokea, tuendelee na kazi hapo kesho"
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal walionekana kumtia moyo huku wengine wakimtaka astaafu kwani umri wake umesogea sana.
Kocha Arsene Wenger aligoma kuzungumzia suala la Cech " Beki yetu haikuwa katika kiwango kizuri , siwezi kuzungumzia goli la pili na la tatu. Swansea walikuwa haraka , makini  na hasira , sisi hatukuwa makini na mchezo wetu.
Kwa matokeo hayo Arsenal inaendelea kubaki nafasi ya 6 nyuma ya Tottenham kwa alama 3 wakiwa na mchezo dhidi ya Manchester United jumatano hii.

Post a Comment

0 Comments