advertise with us

ADVERTISE HERE

MANCHESTER YAFANIKI KUMSAJILI BEKI KISIKI WA BILBAO

Klabu ya Manchester City imetangaza rasmi kumsajili beki Aymeric Larpote kutoka Athletic bilbao kwa dau la paundi milioni 57.
 Mnchester City wamekuwa wakimwania mchezaji huyo tangu msimu wa majira joto na sasa imefanikiwa kupata saini ya beki huyo wa kifaransa. Bei ya Laporte  imevunja rekodi ya usajili na kuwa mchezaji ghali zaidi katika klabu hiyo akimpiku Kelvin De bruyne aliesajiliwa kwa dau la paundi milioni 55 mwaka 2015 akitokea Wolfsburg.
Kupitia mtandao wa manchestercity.com Laporte alisema " nimefurahi kuwa hapa, City ni klabu yenye mipango mingi na ni moja ya klabu kubwa Ulaya. Naungana na kocha Pep Guardiola kuisaidia timu kufikia malengo yake. Klabu imeonyesha kuniamini na kunisajili nimefurahishwa pia kuwa hapa"

Kwa upande mwingine kocha wa Manchester ameonekana kutumia kiasi kikubwa cha fedha tangu kuwasili kwake miezi 18 iliyopita, ametumia kiasi cha paundi milioni 400 huku kiasi cha paundi milioni 190 akitumia kwa usajili wa mabeki tu.
Mapema leo msemaji wa Manchester City alitangaza kumsajili beki huyo " tunatangaza kumsajili Laporte ni mchezaji mzuri tuliyekuwa tukimfuatilia kwa muda mrefu, kwa ubora wake tunaamini ataendana na mfumo wa kocha Pep Guardiola "
Mapema wiki  hii Laporte aliwaaga wachezaji wenzake na mashabiki  wa Athletic Bilbao kwani wamekuwa pamoja tangu mwaka 2012
Lacorte alisema "Napenda kuwashukuru uongozi na wachezaji wa  Athletic Bilbao, nilifika hapa nikiwa kijana mdogo na kufanikiwa kukua vyema nikiwa hapa, kwa sasa naenda kukabiliana na changamoto mpya . sitamani kuondoka ila imenibidi naamini nitarudi siku moja.
Beki huyo atakabiliwa na kupigania namba pamoja na Otamendi, Kompany pamoja na John Stones.
"

Post a Comment

0 Comments