BETI NASI UTAJIRIKE

LUCAS MOURA AWASILI LONDON KUKAMILISHA USAJILI NA KLABU HII

Klabu ya PSG imefungua milango ya kumuuza kiungo wake Lucas Moura kwa dau la Paundi milioni 25.
 Manchester united ilihusishwa kumtaka mchezaji huyo na tetesi hizo ziliota mbawa. kwa sasa mchezaji huyo anategemea kujiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs. Asubuhi ya leo Moura alionekana jjijini London na amehusishwa kufika mazoezini katika klabu hiyo.
 
Mchezaji huyo mwenye miaka 25 alihusishwa kuzungumza na klabu hiyo kuhusu mikataba yake mipya na PSG imeshatoa kibali kwa staa huyo kuondoka.
Mchezaji huyo alijiunga na PSG mwaka 2013 akiisaidia klabu hiyo kubeba mataji manne ya ligi (Ligue 1) na mengine matatu ya the coupe de france. mchezaji huyo ameisaidia timu ya taifa Brazil kwa kufunga mabao 36. 
Msimu huu umekuwa ni mbaya kwa kiungo huyo na amecheza mechi sita tu za ligi. uwepo wa Neymar , Mbappe, Di maria imekuwa kikwazo kwa mchezaji huyo.
Wikiendi iliyopita Pochetino alitangaza kutaka kumsajili mchezaji bora na Moura anahusishwa na dili hilo kwa asilimia 100.

Post a Comment

0 Comments