Kapteni na mfungaji tegemezi wa Inter milan amekoleza zaidi moto na kulaimisha kuhamia Real Madrid kwa lazima
Real Madrid wameonyesha nia ya kutoa euro milioni 110 kumnasa mshambuliaji namba moja wa Serie A. Mchezaji huyo mwenye miaka 24 ameishawishi Real Madrid kwa kuufnga magoli 18 ya ligi msimu huu. Mbali na Real Madrid mchezaji huyo ametolewa macho na vilabu tofauti.
Kupitia mtandao wa instagram mchezaji huyo aliandika "kusema kwaheri ni kukua"
Mke wa Icardi ndio meneja wa mchezaji huyo na alimnukuu akisema "kusema kwa heri ni kukua" wakiweka emoji za kwaheri katika status.
Uongozi wa Intermilan umekana kupokea ofa yoyote kutoka Real Madrid wala klabu nyingine na wanaamini mchezaji huyo atabaki na klabu hiyo. Yakiwa yamesalia masaa 32 lolote linaweza kutokea kwa kuwa dau hilo ni kubwa sana na Inter Milan wanaweza muuza staa huyo.
Jambo jingine linalochangia Icardi kutoendelea na klabu hiyo ni mwenendo wa timu hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri tangu mwezi disemba 3 na inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi.
0 Comments