advertise with us

ADVERTISE HERE

DILI LA MANCHESTER NA ALEXIS SANCHEZ LAOTA MBWAWA

Manchester haikuwa tayari kutoa paundi milioni 20 kwa Sanchez aliebakiza miezi 6 katika mkataba wake na Chelsea wameona ni fursa ya kumpata.
 Klabu ya Manchester City imejitoa kwenye mbio za kumsajili mshambuliaji huyo wa Arsenal. Arsenal pekee inahitaji dau la paundi milioni 20 kwa ada ya uhamisho, wakala wake anahitaji milioni  5 na kukamilisha usajili itatumia paundi milioni 60 .
Mwenyekiti wa Manchester City bwana Mubarak alizungumza na Pep Guardiola na kumweleza fedha hizo ni nyingi mno kwa klabu.
Guardiola amemkosa mchezaji huyo na mpinzani wake wa karibu Jose Mourinho anapewa kipaumbele kumsajili staa huyo wa Chile
Taarifa za ndani zinasema Sanchez anategemewa kuwasili  Manchester United kwa vipimo vya awali. Sanchez anataka kulipwa mshahara wa paundi 275000 kwa wiki na United imeonyesha nia ya kumlipa kiasi hicho. kwa upande mwingine  Chelsea wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo na Conte ila hayupo tayari kumlipa wakala kiasi cha paundi milioni 5.
Arsenal ipo tayari kumtoa mchezaji huyo baada ya mkataba wake kubakiza miezi 6 tu. Dalili za awali zilionekana wikiendi iliyopita, Sanchez hakujumuishwa katika kikosi kilichokwenda Bournemouth City na walifungwa 2-1 na timu hiyo.
 Kocha Arsene Wenger alipoulizwa ni kwanini amemuacha Alexis Sanchez kwenye kikosi chake alisema " Lolote linaweza kutokea kwa sasa, inaweza kuwa leo, kesho ama isiwepo kabisa. ndio maana sikumchagua, sikutaka asafiri pamoja nasi kwa kuwa amebakiwa na muda mchache wa kuondoka na itaamuliwa muda wa masaa 48 yajayo. ilimpa wakati mgumu lakini hakukataa kucheza" alimaliza wenger

Post a Comment

0 Comments