advertise with us

ADVERTISE HERE

CHELSEA YASAJILI STAA MPYA KUTOKA ARSENAL

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa Arsenal kwa mkataba wa miezi 18 kwa dau la paundi milioni 18
 Giroud ameondoka klabuni hapo na kujiunga na Chelsea kwa dau la Paundi milioni 18. Mfaransa huyo atakwenda kugombania namba na Alvaro Morata.
Giroud ameshindwa kutamba msimu huu akiwa Arsenal na mara nyingi kocha wenger amekuwa akimtumia  Alexandre Lacazette.
Ujio wa Aubameyang imekuwa chachu ya staa huyo mwenye miaka 31 kuendelea kubaki Gunners.
Giroud akiwaaga mashabiki wa Arsenal
Mchezo dhidi ya Swansea  ulikuwa  wa mwisho kwa staa huyo klabuni hapo.
Kwa klabu ya Chelsea ni baraka na bahati kwao kumnasa staa huyo. Msimu huu Chelsea imekwa na wakati mgumu kumpata mbadala wa Diego Costa, mbali na uwepo wa Alvaro Morata Chelsea inahitaji staa mwingine mwenye uzoefu kama Giroud.
Andy Carol alihusishwa kuhamia klabuni hapo ila majeraha yamemzuia kusainiwa , baadhi ya wachezaji wengine waliokuwa wanatazamiwa ni Peter Crouch na Eden Dzeko.
Baada ya kujiunga Chelsea Giroud alisema " Chelsea ni moja  klabu kubwa katika ligi kuu ya Uingereza.na ni timu iliyoshinda zaidi taji la ligi kuu kwa miaka sita au saba iliyopita. najivunia kusainiwa na klabu hii na naelekeza nguvu kuitumikia klabu hii.
Mkurugenzi wa Usajili Chelsea alisema" Giroud ni mchezaji aliedhihirisha uwezo wake na tunafuraha kumsajili, amekuwa akifunga magoli na kucheza vizuri pia ana uzoefu na ligi kuu Uingereza , tunaamini usajili wake ni lulu kwa klabu".

Post a Comment

0 Comments