Klabu ya Chelsea imefanikiwa kumnasa beki Emerson kutokea Roma kwa dau la Paundi milioni 23
Beki huyo mwenye miaka 23 akiitumikia timu ya taifa Brazil amefanikiwa kupata mkataba wa miaka minne na nusu.
"nimekuja hapa kwa kuwa ni klabu kubwa yenye historia, leo nimetimiza ndoto zangu za kuchezea moja ya klabu kubwa duniani"
"nimekuwa nikiangalia ligi kuu Uingereza tangu nikiwa na miaka 15 , ni nzuri na ushindani ukiiangalia ila ni nzuri zaidi kama utaicheza pia"
Chelsea ilihusishwa kumtaka beki wa Juventus lakini iliahirisha na kumchukua Emerson.
Mkurugenzi wa Chelsea Bi Marina Granovskaia amepongeza usajili wa Emerson na kusema utaongeza ushindani.
Emerson atavaa jezi namba 23 na atakabiliwa na ushindani wa namba dhidi ya Michael Alonso kwa upande wa beki wa kushoto. pia atacheza ligi ya mabingwa ulaya msimu huu kwani hakuhusishwa na Roma katika kikosi chao kilichoshiriki.
Emerson alianza soka la kulipwa mwaka 2012 na alitolewa kwa mkopo Palmero kabla ya kujiunga na Roma mwaka 2015.
Bi Marina Granovskaia aliongeza" tunamkaribisha Emerson katika klabu yetu, ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee na tunaamini atatusaidia katika mashindano mbalimbali msimu huu"
Chelsea ilitaka kumhusisha Edin Dzeko katika sakata la Emerson lakini mahitaji ya kimkataba yalikuwa tofauti.
Conte anahangaika kupata mshambuliaji mpya yakiwa yamebaki masaa machache ya dirisha dogo kufungwa na anaamini kumpata Giroud wa Arsenal.
Kama usajili wa Aubemayang kutua Arsenal utafanikiwa Giroud ataelekea Chelsea na Batshuayi ataelekea Dortmund.
0 Comments