Mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo amefanikiwa kupata mtoto wa kike afahamiakae kwa jina la Alana Martina.
Kupitia mtandao wa Instagram Ronaldo alidhibitisha kuzaliwa kwa mtoto huyo. Ronaldo na Georgina Rodriguez wamekuwa na uhusiano kwa mwaka mmoja sasa na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.
Ronaldo amezaa watoto watatu kabla ya kuwa na Georgina mwenye miaka 22
Georgina aliwahishwa mapema hospital jumapili jioni tofauti na siku tisa zilizotabiliwa na vyombo vya habari .katika uzinduzi wa nguo zake Ronaldo alihojiwa kuhusiana na watoto wake "kuwa baba ni jambo jema na safari ya kila mtu jambo hili liebadilisha kabisa maisha yangu, limenifundisha kuwa na upendo ambao haukuwepo, imenifanya kuwa na furaha na niko tayari kuwa baba tena , jambo jema ni kuona watoto wanakua na kupata mahitaji yao yote bila usumbufu wowote.
Kukaa nao , kufurahi nao ni moja ya vitu vinavyonipa furaha " alisema nyota huyo wa dunia aliejishindia tuzo ya FIFA PLAYER OF THE YEAR kwa mara ya pili mfululizo akiwamwaga Lionel Messi na Neymar JR.
0 Comments