BETI NASI UTAJIRIKE

BIFU LA HAZARD NA MOURINHO LAFIKA PABAYA

Imefahamika  Kocha wa zamani Chelsea Jose Mourinho na mchezaji wa Chelsea  Eden Hazard wameonekana kutokuwa na uhusiano mzuri. 
 Hilo limefahamika katika mchezo kati ya Chelsea na Manchester United, Mourinho aliwapa mikono wachezaji wote wa Chelsea ila alipokaribia Eden Hazard Mourinho aliingiza mikono mfukoni na kujifanya hamuoni Hazard. mchezaji huyo alipomkaribia Mourinho hakumtazama usoni na alimpita kama hamuoni.
Kabla ya mchezo kuanza Hazard alisema "wakati Mourinho anakuja Chelsea alijitahidi kunifanya niwe mchezaji bora wa Uingereza na aliliweka akilini, nilianza kucheza vizuri kila mchezo na nikafanikiwa kuwa mchezaji bora wa msimu"
Mchezaji huyo wa Ubelgiji alifanikiwa kutwaa tuzo ya PFA na huu ulikuwa  msimu  wa kwanza kwa Jose Mourinho kurejea Chelsea na kushinda kombe la ligi.
Ugomvi wao ulianza  Mourinho aliposema  Hazard hajui kukaba na hilo lilionekana ni uzalilishaji kwa nyota huo.
Katika mchezo huo Chelsea waliibuka na ushindi wa bao 1 kupitia kwa Morata.
Mshambuliaji huyo alisajiliwa kutoka Real Madrid msimu huu na amefanya vizuri tofauti na ilivyotarajiwa kwa kufunga magoli 8 katika michezo 9 aliyocheza.

Post a Comment

0 Comments