advertise with us

ADVERTISE HERE

UGOMVI WA HERRERA NA MOURINHO WAMALIZIKA

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho na kiungo wake Herrera wamemaliza ugomvi wao  mapema leo. chanzo cha ugomvi huo ni Herrera kucheza chini ya kiwango katika mchezo dhidi ya Hudderfield 
 Katika mchezo huo Herrera alicheza chini ya kiwango. kocha Jose Mourinho alikasirika baada ya mchezaji huyo kutofuata maelekezo aliyopewa na kupelekea kupoteza mchezo wao dhidi ya Hudderfield. Baada ya kushinda katika mechi ya kombe la ligi dhidi ya Swansea  Mapema leo herrera amefuatwa na waandishi na kuzungumzia hali ilivyo kiuhusiano na Jose Mourinho

"Ninafuata kila kitu kocha anachosema ,tuna uhusiano mzuri na sasa tunataka kusonga  mbele zaidi, kama ulinisikiliza jumamosi nilivyosema katika dakika 30 Hudderfield walikuwa bora zaidi yetu , ni kweli tulikwazika baada ya kupoteza mchezo ila tumefanya vizuri dhidi ya Swansea"
" tulihitaji kujipanga upya kwa michezo inayofuata na tumefanya hivyo dhidi ya Swansea na katika mchezo huo tumeshinda huku kila mmoja akicheza vizuri kwa nafasi yake. ni mwanzo mzuri na tunajiandaa kuwakabili Tottenham jumamosi" alisema Herrera.
Tottenham inashika nafasi ya tatu katika ligi nyuma ya Manchester United na wamepishana magoli tu pointi kulingana  sawa.Tottenham  hawajapoteza mechi yoyote ugenini msimu huu
Herrera aliongeza" Huo ni mchezo mzuri kwetu na tumejiandaa vizuri, mashabiki wanatakiwa wafahanu bila wao hatuwezi kufanya vizuri , Tottenham wanafanya vizuri kwa misimu hii miwili na wamekuwa wapinzani wetu, wamefanya vizuri dhidi ya Liverpool na Real Mdrid na ni timu inayocheza kwa ushirikiano"
" utakuwa mchezo mgumu kwa pande zote mbili ila tunaamini tutafanya vizuri tukiwa nyumbani na mashabiki watatuunga mkono"


Post a Comment

0 Comments