BETI NASI UTAJIRIKE

STAA WA CHELSEA KUTUA BARCELONA

Klabu ya Barcelona imeanza kumtafuta mrithi wa Jordi Alba anayeondoka mwezi januari ama mwishoni mwa msimu huu
 Baada ya tetesi za Jordi  Alba kujiunga na manchester United klabu ya Barcelona imeweka wazi nia ya kumtaka beki wa  Chelsea  Marcos Alonso.  Taarifa za ndani zinasema Barcelona wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo kwa karibu na kuridhishwa na mwenendo wake.
Beki huyo mwnye miaka 26 alisajiliwa msimu wa 2016/17 kwa dau la paundi milioni 25 akitokea Fiorentina. Mwanzoni alitiliwa mashaka  na kocha Antonio Conte katika mechi dhidi ya Bolton na Sunderland ikidhaniwa hataweza mudu ligi kuu ya Uingereza lakini baadaye mchezaji huyo alirudi katika kiwango chake na kuisaidia Chelsea kubeba kombe la ligi.
Baada ya kiwango kizuri anachozidi kukionyesha Barcelona wapo tayari kutoa dau lolote kwa Chelsea kumnasa beki huyo.

Post a Comment

0 Comments