Kocha wa Manchester United anakabiliwa na upungufu wa mabeki wa kushoto. hivyo ameweka wazi nia yake kuwasajili wachezaji watatu akiwemo Jordi Alba wa Barcelona, Aaron wa Espanyol na Sessegnon wa Fulham.
Majeraha yanayowakumba mara kwa mara Luke shaw, Marcos Rojo, Daley Blind na Ashley Young yamekuwa kikwazo kwa Manchester United. timu hiyo imepanga kumtoa kinda mmoja mwezi januari kupisha usajili wa beki mmoja. Jordi Alba ni moja ya mabeki wenye uwezo mkubwa na tayari maskauti wa Manchester United wameanza kumfuatilia kwa karibu mchezaji huyo.
Manchester United imeanza mazungumzo na timu ya Espanyol kumtaka beki wa kushotoAaron Martin na klabu hiyo imepeleka of ya Euro milioni 35.5 kuweza mnasa beki huyo.
beki huyo wa hispania amecheza michezo 30 msimu uliopita na kuisaidia timu ya Espanyol kubeba kombe msimu wa 2016. katika ngazi ya timu ya taifa Aaron amecheza michuano ya U16, U17, U18, U21 na amekuwa akifanya vizuri.
Manchester city nao wameingia katika mbio za kumfukuzia beki huyo mwenye miaka 21 na mkataba mpaka mwaka 2020. Espanyol watataka dau kubwa zaidi kumuuza mchezaji huyo.
Beki Ryan Sessegnon wa Fulham ni moja ya wachezaji wanaowaniwa na Jose Mourinho mwezi January.
Maskauti wa manchester United wamekuwa wakimfuatilia mchezaji huyo kwa muda mrefu na wanaamini sasa ni wakati sahihi wa kumsajili
0 Comments