advertise with us

ADVERTISE HERE

SANCHEZ KUTUA MANCHESTER MWEZI JANUARI

Imefahamika Arsenal iko mbioni kumtoa nyota wake Alexis Sanchez kwa dau la paundi milioni 30  na klabu za Manchester zinapewa nafasi zaidi.
Nyota huyo mwenye miaka 28 anahusishwa kujiunga na Manchester city na amebakiwa na mkataba wa miezi sita tu akiwa na Arsenal. endapo hatauzwa mwezi januari  Sanchez atatua Manchester city bure na hilo litakuwa suala gumu kwa Arsenal kumruhusu  aondoka bure.
Wiki hii Snachez aliposti picha akiwa na huzuni na haikufahamika ni nini kilimfanya asiwe na furaha lakini baadhi ya wadadisi wanasema Sanchez hana furaha kuitumikia Arsenal.

Habari za ndani Manchester city imeandaa kiasi cha Paundi milioni 20 kumnasa mchezaji huyo mwezi januari na Arsenal wanataka kumuuza kwa paundi milioni 30. Pep anataka kuonyesha utofauti kati ya ligi kuu na ligi ya mabingwa ulaya kufaulu na kushindwa. tunafahamu Sanchez anataka kuondoka na tunaamini tutampata tu. kilisema chanzo hicho.Mchezaji huyo pia anahusiswa kujiunga na  PSG au Manchester United
Mchezaji huyo ameichezea Udinese na Barcelona, mwaka 2014 aliuzwa kwa paundi milioni 31.4 kwenda Arsenal na alifunga goli dhidi ya Everton kwa ushindi mnono wa 5-2

Post a Comment

0 Comments