BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID:LETENI DE GEA TUWAPE BALE

Manchester United inaihofia Real madrid kumchukua De Gea kukamilisha uhamisho wa Bale 
Kocha wa Manchester united na mwenyekiti msaidizi Ed wood wanaamini Gareth Bale atatua klabuni hapo msimu ujao.
 Lakini kuna hata ya kumpoteza kipa wao mahili David de Gea kama watataka kumnasa Gareth Bale. Kipa huyo aliyeibuka mchezaji bora wa klabu kwa misimu mitatu mfululizo huku akitajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Ballon d'or amekuwa akifuatiliwa kwa ukaribu na magwiji wa soka Real Madrid na dili hilo litafanikiwa endapo Bale atatua Manchester United.
 Katika mchezo dhidi ya Liverpool De Gea alionyesha umahili wa hali ya juu baada ya kuzuia mashuti kadhaa. Kwa upande wa Madrid Gareth Bale anasumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara lakini Manchester inaamini ni mchezaji sahihi kwa timu hiyo.

Mwanzoni mwa msimu huu Manchester United ilikutana na Real Madrid katika mchezo wa UEFA super cup na Jose Mourinho alimtania Gareth Bale "sitaweza kukununua kwasababu huongei na mimi"

Post a Comment

0 Comments