advertise with us

ADVERTISE HERE

POGBA APONDA USHANGILIAJI WA LINGARD VS SWANSEA

Baada ya kuisaidia Manchester United kusonga mbele kombe la Carabao, Lingard aliwafuata mashabiki wa Manchester United na kucheza staili iliyowashangaza wengi akiwemo Pogba.
Nyota  huyo wa Manchester United amekuwa akifanya vizuri kila anapopata nafasi na juzi aliibuka mchezaji bora wa mchezo kwa kushinda mabao 2 katika mchezo uliomalizika wa 2-0.
Utata ulianza waliporudi chumba cha kubadilishia nguo na Pogba akimponda kwa staili yake ya ushangiliaji. huku akiigiza namna ya kucheza.  video aliyolisambaa  Lingard ikimwonyesha Pogba akiigiza tukio hilo iliwafurahisha mashabiki wa wachezaji hao.
staili hiyo inafanana sana nyimbo moja wapo ya drake aliyoiachia hivi karibuni katika uzinduzi wa albam yake mpya.
Lingard ni nyota wa miaka 24 anaeichezea Manchester United tangu utotoni, ameisaidia timu hiyo kunyakua makombe kadhaa na kufunga magoli 14 tangu aanze kuichezea Manchester United.

Post a Comment

0 Comments