advertise with us

ADVERTISE HERE

MOURINHO KUSAINI DILI JIPYA NA MANCHESTER UNITED

Klabu tajiri ulimwenguni Manchester United  inajiandaa kumpa mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 65 kocha wake Jose Mourinho.
 Klabu hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya kuridhishwa na mipango na maendeleo tangu awasili Mourinho.
Jose mourinho alijiunga na manchester united mwaka 2016 kwa mkataba wa miaka mitatu  lakini bodi ya wakurugenzi wamevutiwa na uwezo wake baada ya kuisaidia timu hiyo kunyakuwa mataji matatu likiwemo taji la mabingwa ulaya (EUROPA)
Mourinho mwenye umri wa miaka 54 anafungana na mpinzani wake Guardiola huku wote wakilipwa paundi 250,000 kwa wiki lakini nyongeza zaidi kwa mourinho atakapopata makombe.
mkataba huo unaotarajiwa kusainiwa hivi karibuni umeongezwa vipengere ambavyo mpaka sasa vinajadiliwa.
Mwenyekiti msaidizi wa Manchester United bwana Ed woodward ndiye aliependekeza mkataba wa mourinho kuongezwa.
Mourinho ndiye kocha wa kwanza kuipa Manchester United Ubingwa wa EUROPA LEAGUE na kuifanya timu hiyo kuwa na vikombe vinne vya ulaya.

Post a Comment

0 Comments