Ashley Young alitakiwa kuondoka mwezi januari lakini anabaki kutokana na uwezo aliouonyesha hivi karibuni kucheza kama beki
Ashley Young amenusurika kuuzwa mwezi januari mwakani baada ya kuonyesha umahili katika nafasi ya beki wa kushoto. Winga huyo wa zamani wa timu ya taifa Uingereza alijikuta katika wakati mgumu msimu uliomalizika baada ya kuanza michezo miwili kati ya 18.
Kocha Jose Mourinho anasema" mchezaji ninaemngojea kwa maamuzi ni Ashley Young, nimchezaji nimpendae na sitajiskia vizuri akiondoka, ila ni mchezaji pekee niliyepewa taarifa anatakiwa kuondoka.
Kocha Jose Mourinho aliamua kumtumia Ashley Young katika baadhi ya mechi kutokana na kuwakosa baadhi ya mabeki wake wa kushoto Marcos Rojo na Daley Blind. kocha huyo amefurahishwa na mchezaji huyo na anampango wa kumbakiza klabuni hapo.
" nilikuwa sijawahi kucheza kama beki,lakini nimejifunza kwamba mchezaji mahili ni lazima ajifunze kucheza nafasi mbalimbali uwanjani" alisema Young.
takwimu za Ashley Young hivi karibuni.
Mourinho amevutiwa na Ashley Young hivi karibuni na alimpa nafasi ya ukapteni katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya. mwaka 2016 Young alianza katika michezo 7 na kucheza dakika 766 katika mechi 14 akigunga goli moja. mwaka 2017 Ashley Young amecheza michezo 21 akianza mara 17 na jumla ya dakika 1495 na hajafunga goli lolote.
0 Comments