advertise with us

ADVERTISE HERE

MESSI : CHUMA CHA TATU KINAKUJA

Baada ya Thiago na Matteo Lionel Messi na Mkewe Antonella Raccuzzo wanategemea kupata mtoto mwingine

Kupitia mitandao wa kijamii Roccuzzo mke wa Lionel Messi amepost picha akiwa na watoto wawili pamoja na Messi na kuandika Family  de 5 akimaanisha Familia ya watu watano. kauli hiyo inamaanisha ni mjamzito.
Wiki hii imekuwa nzuri kwa Lionel Messi baada ya kushinda hat trick na kuisaidia Argentina kufuzu kucheza kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Kwa upande wa mpinzani wake Cristiano Ronaldo nae hayuko nyuma na kuonekana kushindana  kila kitu na Lionel Messi, kuanzia Uwanjani, Matangazo ya Biashara mpaka Kitandani baada ya Ronaldo nae kuwahi posti akielezea ujio wa mtoto wake wa 4.
Kupitia Instagram Ronaldo aliandika Family mood. Ronaldo mpenzi wake Georgina Rodriguez wanategemea kupata mtoto mwingine na ronaldo kuwahi post " another baby on the way" akimaanisha mtoto wanne anafuata.
Messi na Ronaldo wanabaki kuwa wachezaji Bora kwa kipindi cha miaka 10 kwa kupokezanna tuzo za Ballon 'd or Messi akichukua mara 5 na Ronaldo mara 4 na mwaka huu wametajwa tena kuwania tuzo hizo na wanapewa nafasi ya kubeba tena.

Post a Comment

0 Comments