advertise with us

ADVERTISE HERE

MASTAA MANCHESTER UNITED WAREJEA KUIKABILI TOTENHAM

Ibrahimovich amerejea dimbani baada ya kupona majeraha ya goti. mchezaji huyo ameonekana mazoezini na wachezaji wenzake.
 Kupitia mtandao wa kijamii, Ibra aliposti picha akiwa na Bailly pamoja na De Gea. alionekana kumwekeza mkono Bailly na  kuandika "hawezi kukimbia tena"
Ibra aliumia tangu mwezi aprili 20 na alifanyiwa upasuaji. kwa sasa Movich anaonekana kuwa fiti kwa michezo inayofuata.
Ibramovich amecheza michezo 46 na kufunga magoli 28 akiwa na Manchester United kwa msimu uliopita.
Ijumaa iliyopita Mourinho alisema" Ibrahimovich amerejea na ataanza mazoez. ni mchezaji anaefanya vizuri na ameshaanza mazoezi ya viungo na mwaka huu 2017 ni lazima aanze kucheza"
Movich amejiunga na manchester United katika mazoezi na amekuwa akicheza kwa dakika 20-25 kuanza kumweka fiti.
Kwa upande mwingine beki Eric Bailly naye ameendelea na mazoezi na anategemewa kanza katika mchezo dhidi ya Tottenham wikiendi hii.

Post a Comment

0 Comments