BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER UNITED KUMWAGA FEDHA TENA KWA KIUNGO MPYA

Manchester United na Valencia wamefungua mazungumzo maalumu kwa ajili ya kiungo Soler mwenye thamani ya paundi milioni 30.
 Jose Mourinho ana Fellain, Carrick na Herrera ambao wote mikataba yao inakaribia kumalizika msimu ujao.
Tangu mazungumzo ya kumnunua mchezaji huyo mwenye miaka 20 yaanze yameonekana kuleta mafanikio na manchester United inajiandaa kumsajili mchezaji huyo msimu ujao.
Katika mkataba wake na Valencia Soler anatakiwa kuuzwa ka paundi milioni 75. Kiungo huyo amefanya vizuri katika kikosi cha pili kwa misimu miwili mfululizo na sasa Manchester United inamtolea macho.
Soler alipoulizwa kuhusu tetesi za kujiunga na Manchester United alisema "Hicho ni kitu kinachofanywa na timu pamoja na wakala, ninapoingia uwanjani huwa sifikirii masuala ya kuuzwa ingawa mkataba wangu unaonyesha nina thamani kubwa".
Kama kinda huyo atatua United basi atachukua mikoba ya Michael Carrick anaestaafu msimu huu mwishoni.

Post a Comment

0 Comments