Kocha msaidizi wa simba ameamua kuachana na Simba na kurejea nchini Uganda. Vyanzo vya ndani havijatoa sababu za msingi kwa kocha huyo kuondoka
Kocha Mayanja hajaonekana mazoezini kwa siku mbili mfululizo hali iliyozua sintofahamu kabla ya kocha huyo kuaga rasmi klabuni hapo kwa kudai ana matatizo ya kifamilia.
Hilo ni pigo kwa Simba kwani kocha huyo na Omog wameisaidia vyema Simba msimu huu kwa kuongoza ligi na kutofungwa mechi yoyote.
Simba inajiandaa na mchezo dhidi ya Njombe mji utakaopigwa wikiendi hii katika uwanja wa Uhuru.
0 Comments