Kocha Arsene Wenger amekiri kuchanganywa na mwenendo mbaya wa Arsenal na kuhofia kuwapoteza bure mastaa wake wawili
Wenger atalazimika kuwauza Mesut Ozil na Sanchez mwezi January kutokana na mikataba ya wachezaji hao kuwa na kikomo mwishoni mwa msimu huu. Wenger amekiri kupokea ofa kumtaka Sanchez lakini kwa Ozil hajapokea ofa yoyote ilihali wote wamebakiza miezi nane ya kubaki Gunners ama wataondoka bure.
Manchester city inaasilimia 90 kumchukua Sanchez na Pep Guardiola alionyesha nia kumtaka mchezaji huyo.
Klabu nyingi zimeshindwa kumfuatilia Mesut Ozil mwenye miaka 29 akitaka kulipwa Euro 330,000 kwa wiki. Arsenal inatafuta timu ya kumnunua Ozil lakini wengi wamekiri mshahara huo ni mkubwa ingawa Inter milan wameonyesha nia.
Taarifa za ndani zinasema hakuna maelewano mazuri kati ya Wenger na Ozil tangu mchezaji huyo agome kusaini mkataba mpya na Wenger akimlalamika kutojituma katika timu.
Arsenal imeachwa point 9 na Manchester city na imekubali kupigwa mechi tatu mpaka sasa.
0 Comments