advertise with us

ADVERTISE HERE

KANE KUVUNJA REKODI YA NEYMAR

Thamani ya Kane imetangazwa kwa klabu yoyote inayotaka kumnunua kutoka Tottenham hotspurs na itaweka rekodi ya dunia.
 Mchezaji huyo anatajwa kuwa na thamani ya Euro milioni 250 na kama atafanikiwa kununuliwa kwa dau hilo basi atavunja rekodi ya Neymar Jr aliehamia PSG kutoka Barcelona kwa dau la Euro million 222.
Real Madrid inaonekana kupewa kipaumbele kumchukua mchezaji huyo wa Uingereza na Tottenham baada ya kufanya vizuri misimuyote mitatu ukiwemo wa 2017/18 kwa kufunga magoli 13 katika michezo 12.
Kama atajiunga na Real Madrid atakuwa ameungana na wachezaji wenzake wawili waliotokea Spurs akiwemo Gareth Bale alieweka Rekodi ya Dunia kwa kununuliwa kwa Euro milioni 100 na Luka Modrick.
Raisi wa Real Madrid alifanya mazungumzo na Radio moja na alisema" Nafikiri ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na kubwa zaidi ni umri wake unamruhusu kuendelea kucheza kwa muda mrefu"
Perez anaamini ili kumpata mchezaji huyo ni lazima atoe fedha nyingi zaidi ya euro milion 222 aliyosajiliwa Neymar Jr.
" sijaulizia thamani yake na najua n nikiuliza atasema kiasi cha euro milioni 250." aliongeza Perez.
"Tuna urafiki wa kibiashara na Totenham tangu kumnunua Bale na Modric na yote yalifanyika dakika za mwisho kabisa"
"Mimi na Levy (raisi wa Totenham) tunamawasiliano mazuri na hata tuliposhinda ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya alinipongeza kwa kusema "hongera kwa ubingwa kupitia wachezaji wangu"
Kane amefanikiwa kuonyesha uwezo kwa Real Madrid kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya uliomalizika kwa sare ya1-1 na watakutana tena novemba 1 Wembley.

Post a Comment

0 Comments