advertise with us

ADVERTISE HERE

IWE MVUA LIWE JUA LIVERPOOL KAZI KAZI

Klopp ameonekana kucharuka baada ya kufungwa 4-1 na Totenham. Mbali na kwamba kuna mvua kali wachezaji wa Livepool  wameonekana kufika mazoezini kujiandaa na michezo inayofuata ukiwamo dhidi ya Hudderfield  wikiendi hii
  Kocha Jurgen Klopp akiwasili mazoezini na gari yake aina ya Melwood. Liverpool inajiandaa kukabiliana na timu iliyopanda daraja  msimu huu Huddersfield. Timu hiyo iliishangaza dunia baada ya kuifunga Manchester United bao 2-1 na sasa inajiandaa kukabiliana na Livepool uwanja wa Anfield.
Simon Mignoret aliwasili mazoezini hapo na gari aina ya Audi Q7
Emre Cans aliwasili mazoezini na Bentley Continental
Dejan Levron alifika mazoezini na gari yake aina ya Range Rover sport
James Milner alifika mazoezini hapo na gari aina ya BMW 4X4
Msimu huu safu ya ulinzi ya Liverpool imeonekana kuwa mbovu zaidi baada ya kuruhusu magoli 16 kufungwa katika michezo 9.
Vipoigo viwili vikubwa ilivyovipata dhidi ya Manchester city 5-1 na Totenham 4-1 vinamweka mashakani kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp. Taarifa za ndani zinasema kama Klop ataendelea kufungwa kuna uwezekano akaachia nafasi yake na kuchukuliwa na kocha mwingine. Wengi wanadhani Carlo Ancelloti anaweza kuchukua mikoba hiyo baada ya kutimuliwa na Bayern Munich.

Post a Comment

0 Comments