advertise with us

ADVERTISE HERE

CONTE : CHELSEA IMEPOTEZA NAMNA YAKE YA UCHEZAJI

Kocha Antonio Conte amekasirishwa na matokeo mabaya dhidi ya Roma katika mchezo ambao Chelsea ilikuwa imeshashinda
 Conte alimtumia David Luiz kama kiungo na mchezaji huyo aliisaidia Chelsea kupata bao la kuongoza kabla Hazard hajafunga bao la pili. Chelsea walionekana kumiliki mpira lakini Uzembe wa mabeki  ulisababisha Roma kufunga magoli matatu kabla Hazard hajapata goli la kusawazisha. mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3.
Conte amesema "Sipendi aina ya mchezo tunaoucheza hivi karibuni, na ni wakati wa kuchukua maamuzi, najaribu kuilinda timu yangu hasa eneo la kiungo mkabaji, kuna wakati tunapoteza aina yetu ya uchezaji , kuna wakati unajaribu kutafuta mbinu tofauti, unafeli na kufaulu na Roma walistaili kupata matokeo hao"
Chelsea inaongoza kundi C kwa pointi mbili juu ya As Roma na timu hizo zitakutana tena mwezi huu kwa mchezo wa marudiano.
Conte amekiri timu yake inashindwa kufanya vizuri, kukosekana kwa Drink Water, Ng'olo Kante pamoja na Victor Moses kumempa changamoto mpya. habari mbaya zaidi ni kuumia kwa David Luiz alietolewa kipindi cha pili na Gary Cahill aliemaliza mchezo na bandeji kichwani.
HAKUNA LAWAMA
Kocha huyo alisema haoni haja ya kumlaumu yeyote kwani timu hiyo inafahamu ina wachezaji muhimu watatu ambao ni majeruhi, Luiz nae angeongezeka kama angemaliza mchezo , Bakayoko nae alipata maumivu aliyoyapata Luiz. Tulikuwa tunaongoza goli 2-0 ilibidi tubakize point tatu lakini tulishindwa na kuiruhusu roma kurudisha alisema Conte.

Post a Comment

0 Comments