BETI NASI UTAJIRIKE

BARCELONA YAHOFIA KUMKOSA COUTINHO, YAANZA TAFUTA MBADALA WAKE

Klabu ya Barcelona imekiri kupata wakati mgumu  kumpata mchezaji Philipe Coutinho na imeanza mchakato wa kumtafuta mbadala wake.
 Baada ya kumkosa mchezaji huyo kipindi cha majira joto Barcelona wamepanga kurudi tena kwa mchezaji huyo mwezi januari . kama watamkosa tena wamepanga kuwasajili mchezaji Meyer wa Schalke 04 na Brandty wa Bayern Leverkusen.
Habari za ndani Barcelona zinasema klabu hiyo imeanza mazungumzo na uongozi wa Schalke 04 kwa ajili ya kumnasa Meyer mwenye miaka 22 na kumuongeza Brandt mwenye miaka 21 anaekipiga Bayern Leverkusen.
Brandt Meyer  ni moja ya wachezaji waliofanya vizuri katika michuano ya kombe la Mabara nchini Urusi na kuisaidia Ujerumani kubeba ubingwa huo.
Mpaka sasa Barcelona inahangaika kutafuta mbadala wa Xavi aliekwisha staafu na majina haya matatu yanafuatiliwa kwa ukaribu na Klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments