advertise with us

ADVERTISE HERE

ARSENAL,CHELSEA,MANCHESTER UNITED,CITY,LIVERPOOL KUFANYA KUFURU JANUARY

Kuelekea mwezi Januari 2018 baadhi ya vilabu vinajiandaa na usajili. wafuatao ni wachezaji wanaotegemewa kujiunga na vilabu mbalimbali barani Ulaya hasa Uingereza
 1.IKER CASILLAS
Iker Cassilas mwenye miaka 36 anahusishwa kuhamia Liverpool mwezi Januari. kipa huyu wa hispania alikuwa msaada mkubwa kwa timu ya taifa hispania akiisaidia timu hiyo kubeba kombe la mataifa ulaya EURO CUP mara mbili mfululizo na kuipa Hispania kombe la kwanza la dunia, ameisaidia Real Madrid kubeba La Liga na UEFA kabla ya kutimkia FC Porto. Liverpool wanajiandaa kumsaini kipa huyo.
2.MARCO REUS
Kiungo wa Ujerumani na Borrusia Dortmund amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na anajiandaa kutimkia Arsenal na Manchester United ambazo zimevutiwa na uwezo wake.
3.Julian Draxler 
 Uwepo wa mastaa wengi katika klabu ya PSG unamweka katika wasiwasi nyota Draxler na sasa anatafuta klabu itakayomfanya awe na uhakika wa nafasi wakati wote. Liverpool imeonyesha nia ya kutaka kumnunua staa huyo na mwezi januari mambo yatakuwa yamekamilika.
4.MESUT OZIL
 Anahusishwa na kuhamia Manchester United baada ya mkataba wake na Arsenal kufika ukingoni. Kiungo huyu mwenye miaka 29 anataka ongezeko la mshahara na Arsenal haipo tayari kufanya hivyo. taarifa zinasema nyota huyo anahusishwa kuhamia Manchester United ingawa mwenyewe amepinga vikali kauli hizo.
5. ALEXIS SANCHEZ 
 Manchester city wameonyesha nia kumtaka staa huyu wa Arsenal na Chile. kama hatasaini mkataba mpaka mwezi januari nyota huyo atatimkia Manchester city au United huku klabu ya PSG ikionyesha kumtaka nyota huyo.

Post a Comment

0 Comments