advertise with us

ADVERTISE HERE

ARJEN ROBBEN ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Arjen Robben ametangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa Uholanzi baada ya kushindwa kufuzu kombe la Dunia 2018 nchini Urusi
 Mbali na kufunga magoli mawili katika mechi dhidi ya Sweden hapo jana Robben na wenzale wameshindwa
kufuzu michuanoya kombe la dunia nchini Urusi. Uholanzi walitakiwa kushinda magoli 7-0 ili kuweza kufuzu michuano hiyo lakini ndoto yao ilikwama.
Mchezaji huyo muhimu wa Uholanzi mwenye miaka 29 ametangaza rasmi kuachana na timu ya taifa. Robben amekuwa mchezaji tegemezi wa Uholanzi tangu akiwa na miaka 19 akiisaidia timu hiyo kucheza fainali 3 za kombe la dunia na fainali tatu za Kombe la ulaya  amecheza michezo 96 na kushinda magoli 37 kwa timu hiyo.
"kwa sasa naelekeza nguvu zote kwa klabu yangu, na  ni wakati muafaka wa kuibuliwa vipaji vipya" lisema robben.
Moja ya mambo ya Robben kukumbukwa ni mwaka 2010 alipoisaidia timu yake ya Uholanzi kufika fainali ingawa ilifungwa na hispania goli 1-0 hivyo kurejea nyumbani bila kombe
mwaka 2014 walifanya vizuri chini ya kocha Van gaal wakiisambaratisha hispania goli 5-0 na kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Brazil waandaaji wa mashindano.
mwaka 2016 walishindwa kufuzu michuano ya ulaya ngazi ya taifa na mwaka 2018 wataikosa michuano ya kombe la dunia.

Post a Comment

0 Comments