advertise with us

ADVERTISE HERE

ALICHOKISEMA BERBATOV KWA LIONEL MESSI NA RONALDO

Ubishani wa nani bora duniani kwa soka kizazi hichi haujawaacha salama baadhi ya wachezaji akiwemo Berbatov.

Berbatov amecheza timu moja na Cristiano Ronaldo kwa miaka miwili na kuisaidia timu hiyo kushinda taji la ligi kuu. na mwaka 2009 waliingia fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona na Messi alidhibitisha ubora wake katika mchezo huo.
Berbatov amekiri messi ni mchezaji wa tofauti kabisa na wengine aliocheza nao na amekiri uwezo wa Messi ni mkubwa kuliko Ronaldo. alienda mbali zaidi kwa kusema kizazi cha zamani kilikuwa na Pele,Maradona ila kizazi hiki kina Messi na Ronaldo.
Berbatov amesema "ninapoitazama Barcelona ikicheza mara zote najisemea Messi, Messi,Messi, Ronaldo nimchezaji mzuri ila Messi ni tofauti. wachezaji wengi wanaochipukia hupenda kuwa kama Ronaldo,wananyoa kama Ronaldo ama kumiliki magari na kuvaa kama yeye lakini uwanjani wako tofauti kabisa na yeye"
"Tukiwa vyumba vya kubadilishia nguo alikuwa ni mtu wa utani sana pamoja na Patrick Evra nami nilikuwa ni mkimya sana , akiingia uwanjani ni mtu wa tofauti sana anakuwa makini zaidi na hapendi mchezo. huwa nawaambia wachezaji chipukizi Ronaldo alikuwa anajituma mazoezini na hata baada ya mazoezi alikuwa anafanya mazoezi mengi zaidi ndio maana ni bora.
Ronaldo amecheguliwa tena kuwa mchezaji bora katika tuzo za Fifa Football Awards kwa mara ya pili mfululizo akipata kura asilimia 43.5. Maswali mengi yameibuka juu ya tuzo hizo na baadhi ya mastaa akiwemo berbatov ametoa ya moyoni.


Post a Comment

0 Comments