advertise with us

ADVERTISE HERE

WENGER AMPONGEZA LACAZZETE

Kocha Arsene Wenger amefurahishwa na uwezo wa  mchezaji Alexandre Lacazzete  dhidi ya Westbromwich ambapo alifunga mabao mawili yaliyoipa ushindi Arsenal.
Lacazzete ana magoli manne katika mechi 6 za ligi na wenger amekiri mchezaji huyo ana uwezo  wa kipekee. mchezaji huyo kutoka ufaransa amevunja rekodi ya kushinda mechi tatu za mwanzo uwanja wa nyumbani tangu ilivyofanywa hivyo mwaka 1988.
" si mfungaji pekee ni mchezaji anauwezo wa kuunganisha timu,anapigana sana na kujiamini sana na anajitahidi kuendana na mfumo wa timu" alisema Wenger
"Nilimtoa kwa kuwa alikuwa amechoka ila aikuwa na uwezo wa kufunga hat-trick na nilimpa penati pia, kinachotakiwa ni kushinda mchezo na si kucheza kamali kama wangerudisha 2-1 tungekuwa na wakati mgumu" alimaliza kwa kusema wenger.
Arsenal itacheza na BATE Borisov alhamisi hii katika mchezo wa ligi ndogo ya mabingwa ulaya kabla ya kuivaa Brighton & Hove albion jumapili katika mchezo wa Ligi kuu uingereza .

Post a Comment

0 Comments