advertise with us

ADVERTISE HERE

WELBECK ,RAMSEY WANAWEZA KUTIMKA BURE ARSENAL

Kocha wa Arsenal Wenger amekili kuwepo ugumu kuwazuia  kuwapa mikataba  mastaa wa timu hiyo Aaron Ramsey na Welbeck.

Arsene Wenger anahofia wachezaji hao wanaweza kukataa mikataba mipya na kuondoka bure mwaka 2019 kama itakavyokuwa kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil mwishoni mwa msimu huu.
wenger amepanga kuandaa mikataba mipya kwa welbeck na Ramsey lakini  amekiri kupata wakati mgumu k kuwashawishi wachezaji hao.
Mwishoni mwa msimu Sanchez,Ozil,wilshere na Debuchy wataondoka bure  kutokana na mikataba yao kufikia mwisho na wameonyesha dalili ya kutoongeza.
Wenger: Tunataka kuwapa mikataba Danny Welbeck na Aaron Ramsey tatizo ni kiasi kikubwa cha fedha wachezaji wanachodai hivyo tunaweza kwenda mpaka mwisho wa mikataba yao, klabu inajiandaa kutoa bei kubwa za wachezaji au kuwaruhusu kuondoka bure mikataba yao ikiisha"
Wenger aliendelea" msimu huu kuna wachezaji 107 ambao mikataba yao imefika mwisho na klabu nyingi zinataka fedha nyingi kwa timu za kawaida  na wanasema kama mchezaji huyu thamani yake ni paundi milion 200 basi huyu ni paundi milion 50, na kila mtu anajua paundi milioni 50 ni kiasi kikubwa sana cha fedha ,kwahiyo klabu haitauza mchezaji wala kuongeza mkataba kwa mchezaji bora aondoke bure"

Post a Comment

0 Comments