advertise with us

ADVERTISE HERE

VARANE AONGEZA MKATABA MPYA REAL MADRID

Klabu ya Real Madrid imeendelea kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wake na leo hii ilikuwa zamu ya beki machachali Rafael Varane.
Mchezaji huyo ameongeza mkataba wa miaka mitano na kuwepo katika klabu hiyo mpaka mwaka 2022.
Real Madrid ilitangaza "Tumekubaliana na Varane kuongeza mkataba utakaombakisha mchezaji huyo mpaka june 2022"
Madrid imewaongeza baadhi ya mastaa wake mikataba mirefu mpaka mwaka 2022 baadhi yao ni Isco,Marcelo na Dani Carvajal pia imemuongezea mkataba mchezaji wake Karim Benzema mkataba utakao dumu mpaka mwaka 2021.
Kocha wa timu hiyo zinedine zidane nae ameongeza mkataba kuendelea kukinoa kikosi hicho.
ikumbukwe Zinedine zidane akiwa mjumbe wa timu hiyo alihakikisha varane ananunuliwa kutoka Lens mwaka 2011 na mpaka kufikia sasa mchezaji huyo ameshinda makombe 13 yalkiwemo 3 ya ligi ya mabingwa ulaya.
Msimu huu  Varane anazidi kuwa tegemezi zaidi kwa kuondoka pepe na  kucheza vizuri  pembeni ya Sergio Ramos.

Post a Comment

0 Comments