advertise with us

ADVERTISE HERE

SHEARER: BORA RODGERS KULIKO KLOPP

Alan Shearer ameicheka timu ya liverpool kwa ubovu wa safu ya ulinzi na kusema Brendan Rodgers ni kocha  bora kuliko Jurgen Klopp.
 Jurgen Klopp anajikuta akiwa na wakati mgumu kutokana na timu hiyo kuruhusu goli nyingi zaidi msimu huu. katika michezo sita ya ligi liverpool imeruhusu goli 11 na kushinda magoli 12 huku ikiwa imefungwa magoli  katika mechi mbili dhidi ya Sevilla katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya na mabao 2 dhidi ya Leicester city. msimu huu pekee timu hiyo imefungwa goli 15 katika mechi 8 ilizocheza.
 Mchezaji mkongwe na mstaafu Alan Shearer ameamua kumkosoa Klopp na kusema kosa alilolifanya mwanzo wa ligi limeendelea kuwepo mpaka sasa, hakuishia hapo akaendelea kwa kusema bora kocha wa zaman  Brendan Rodgers  kuliko Klopp.

"Nikweli Klopp kawarudisha nafasi za kushiriki ligi ya mabingwa ulaya kitu kilichomuongezea sifa ndani ya klabu lakini Rodgers alifanya vizuri msimu wa 2013-14 ambao liverpool walifunga magoli 101 wakimaliza nafasi ya 2 nyuma ya manchester city aliewazidi goli moja na pointi 2 rekodi iliyoifanya kuwa timu ya tatu kufunga magoli memgi ndani ya msimu 1. pia walifungwa magoli 50 na mengi zaidi ya timu zote zilizoshirika nafasi tano za juu.

 Brendan anaweza kuwa na rekodi nzuri zaidi kuliko Klopp pale Liverpool" alimaliza kwa kusema Allan Shearer.
                  Chati ikionyesha jinsi Klopp na Rodgers katika mechi 73 walizoitumikia timu hiyo

Post a Comment

0 Comments