advertise with us

ADVERTISE HERE

RASMI:CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA DIEGO COSTA

Chelsea imetangaza kumuuza mshambuliaji wake kwenda Atletico Madrid

Klabu ya Atletico Madrid  itatakiwa kutoa zaidi ya euro milioni 50 kumpata mchezaji huyo wa Chelsea . mchezaji huyo kwa sasa yupo jijini madrid kwa vipimo na makubaliano ya mkataba na timu.
imefahamika chelsea haitaendelea kumlipa mchezaji huyo  mara baada ya uhamisho huo kukamilika
Diego Costa anaondoka chelsea kwa kutotakiwa na kocha Antonio Conte na hajaonekana klabuni hapo tangu msimu unaanza.
kauli ya conte ilimfanya Costa asirudi klabuni hapo hapa na alielekea Brazil kabla ya wiki chache kuelekea jijini Madrid.
Chelsea imetangaza rasmi kumuuza mchezaji huyo kuelekea Atletico madrid timu aliyotokea kabla ya kujiunga na miamba hiyo ya London.
Atletico Madrid ilishindwa kumsajili mchezaji huyo  msimu wa majira joto kutokana na kufungiwa kufanya usajili ,Mbali na kusajiliwa huko costa hata ichezea klabu hiyo mpaka Janiuary mwakani klabu hiyo itakapomaliza adhabu hiyo.
Costa hajacheza mchezo wowote kwa siku 98 tangu alipoichezea timu ya taifa Hispania dhidi ya Macedonia  mwezi wa  sita  wakiwania nafasi ya Kucheza Kombe la Dunia.
Costa alifunga magoli 20 katika michezo 35 aliyoichezea klabu ya Chelsea msimu huu na kuisaidia klabu hiyo kubebwa ubingwa wa Uingereza.

Post a Comment

0 Comments