advertise with us

ADVERTISE HERE

POGBA ,DEMBELE NJE MIEZI MITATU

Hali imekuwa tata kwa klabu ya Manchester united  na Bacelona  baada ya nyotawao kupata majeraha makubwa.

Klabu   ya Mancester imejikuta katika wakati mgumu baada ya taarifa za madaktari kuonyesha Paul Pogba anatakiwa akae miezi mitatu akiuguza majeraha aliyoyapata jumanne dhidi ya FFC Basel katika mchezo wa ligi ya mabingwa.
Pogba mwenye umri wa miaka 24 alinunuliwa mwaka  2016 kutoka Juventus kwa dau la paundi milioni 89 na aliisaidia Manchester United kupata makombe matatu na kuibuka mchezaji bora wa Europa.

Vyanzo vya ndani vinasema kuna uwezekano Pogba kukaa nje kwa wiki 12 na vikisema majeraha yake ni makubwa.

klabu inaamini majeraha ya Pogba yametokana na kufanya mazoezi binafsi . na vilisema  " si kawaida kwa mchezaji huyo kufuata ushauri wa kitaalamu kuhusu mazoezi"

Pogba ataelekea marekani kwa matibabu pamoja na wataalamu wa viungo.pogba atakosa mechi 5 za ligi ya mabingwa ulaya , huku akikosa michezo ya ligi kati ya Liverpool Tottenham , Chelsea , Arsenal na Manchester city

kwa upande wa pili klabu ya Barca imepata pigo baada ya mchezaji wake ghali  Ousmane Dembele   \
 kuumia ,Taarifa kutoka Barcelona zinasema Dembele ana jeraha katika mguu wa kushoto na atakaa nje kwa 16.
mchezaji huyo wa miaka 20 alinunuliwa kutoka Borusia Dortmund  kwa ada ya euro milion 145 kulingana na uwezo atakaouonyesha. mpaka sasa mchezaji huyo amecheza michhezo mitatu akiisaidia barca kuifunga Espanyol, kuisaidia timu hiyo kuifunga Juventus 3-0 kabla ya kutolewa nje dakika ya 29 ya mchezo dhidi ya Getafe walioshinda 2-1 .

Dembele atakosa mechi zote za makundi ligi ya mabingwa ulaya na atarudi uwanjani disemba 23 dhidi ya Real Madrid.

pia atakosa michezo miwili ya timu ya ke ya Taifa Ufaransa  kufuzu kombe la dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mwezi ujao

Post a Comment

0 Comments