advertise with us

ADVERTISE HERE

PHELIPPE COUTINHO: SINA MAKUBALIANO NA BARCELONA

Hakuna makubaliano yoyote kati ya coutinho na Barcelona kujiunga na magwiji hao wa hispania .na Coutinho amewahakikishia majogoo wa jiji kuwa yupo hapo kuisaidia timu hiyo.
wiki chache zilizopita coutinho alikuwa na wakati mgumu baada ya uwepo wa mvutano kati yake na klabu katika sakata la kujiunga na Barcelona  kwa dau la euro milioni145.mchezaji huyo mwenye miaka 25 alilazimisha kuondoka lakini uongozi ulimwekea ngumu. msimu huu amecheza dakika 78 tu kati ya michezo sita liverpool iliyocheza, hata hivyo alishindwa kuisaidia klabu hiyo baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Burnley  . Coutinho ameeleza mkasa mzima
" kilichotokea ni ofa ya kazi, na kwenye maisha kuna wakati unakuwa na hamu ya kwenda mahali flani lakini  kuna wakati mambo huwa tofauti, kwa suala langu kila mtu anafahamu nilikuwa nataka  ya kujiunga na Barcelona hata familia yangu inaelewa pia" alisema coutinho.
 aliendelea kwa kusema " ni fursa ya kipekee kujiunga na barcelona lakini pia kuchezea Liverpool ni fursa pia, nimekuwa hapa kwa miaka mitano na sina tatizo na mtu yeyote kuanzia wachezaji wenzangu mpaka uongozi.

Coutinho alipoulizwa kuhusu mstakabali wake kujiunga na Barcelona alikana kwa kusema hakuna lolote linaloendelea kati yake na timu hiyo "nipo sehemu ninayoheshimika nami naheshimu kila mtu alimalizia kwa kusema kwa sasa anaangalia namna ya kuisaidia Liverpool katika kufikia lengo lake.

Post a Comment

0 Comments