advertise with us

ADVERTISE HERE

MANCHESTER CITY YAIANGAMIZA WATFORD, LIVERPOOL YANG'ANG'ANIWA NA BURNLEY

Manchester imeendeleza ubabe wake wikiendi hii baada ya kuibamiza Watford kwa mabao 6-0 huku kun Aguero akiibuka kinara wa ufungaji kwa kupachika mabao matatu na hii inamfanya Aguero kuwa mfungaji  wa kwanza kufunga hat trick msimu huu.
                              
Manchester city walianza mchezo kwa kujiamini na kujipatia goli la kuongoza dakika ya 27 kupitia Aguero aliepokea pasi kutoka kwa Kelvin De Bruyne, Aguero hakuishia hapo kwani alifunga goli jingine kwa pasi murua kutoka kwa david silva, goli la tatu lilifungwa na Gabriel Jesus akipokea pas kutoka kwa Aguero, Nicolas Otamendi aliongeza goli la nne  kisha  Aguero alilludi tena golini kukamilisha hat trick kabla Raheem Sterling  hajafunga kazi.

 City wanaonekana kufanya vizuri wiki hii baada ya kuisambaratisha liverpool mabao 5-0, kisha feyenood  4-0 mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya na ushindi wa leo 6-0 unaifanya timu hii kuwa na jumla ya mabao 15 katika mechi 3 ilizocheza wiki hii. na hii inamfanya Aguero kuongoza wafungaji kwa jumla ya magoli 5 , akifuatiwa na Gabriel Jesus na Lukaku.
naye kocha Pep Guardiola ameonekana mwenye furaha kwa kusema "ilikuwa nzuri ,tumecheza vizuri kama timu hata baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa ugenini, tunafuraha " Guadiola aliongeza "nilikuwa na bahati kuifundisha Barcelona kwa nyakati tofauti lakini sasa tumerudi kwenye aina yetu ya soka"

kwa Upande wa pili liverpool imeonekana kufanya vibaya zaidi wiki hii kwa kuruhusu goli 8 kufungwa na kufunga goli tatu tu, kizaa zaa kilianza mara baada ya kufungwa goli tano na manchester city kisha droo 2-2 dhidi  Sevilla na kudroo tena dhidi ya Burnley. Pengo la Sadio Mane limezidi kuonekana mbali na kwamba coutinho alikuwepo kwa mara ya kwanza uwanjani baada ya kushindwa kujiunga na Barcelona .
 Burnley walianza kwa kujipatia bao kabla ya Salah kusawazisha matoke hayo yameipeleka liverpool nafasi ya 8 matokeo ambayo yalimuuiza klopp na alisema" sina furaha nina hasira na matokeo tulicheza vizuri, ni makosa yetu tuliutawala mchezo ila tukafunga goli moja". kwa sasa liverpool inapaswa kuchunga zaidi nafasi ya ulinzi kwan imeshafungwa goli 11  na kufunga goli 11  katika mechi 6.

Post a Comment

0 Comments