advertise with us

ADVERTISE HERE

FIFA: Refa Aliyeharibu mpira wa Afrika Kusini na Senegali tunamnyoosha


                                   Mechi ya Senegal na Afrika Kusini kurudiwa a novemba-fifa

FIFA imedhibitisha mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Afrika kusini na Senegal kurudiwa mwenzi novemba na maamuzi hayo yamepelekea kifungo cha maisha refa aliechezesha mchezo huo 

shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limedhibitisha kurudiwa kwa mechi hiyo mara baada ya kugundulika kwa makosa ya kiuamuzi yaliyofanywa na refarii Joseph Lamptey. katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Afrika kusini kushinda magoli 2-1.

penati iliyotolewa na bwana Lamptey akidhani mchezaji wa senegali kalidou koulibaly ameushika mpira huo , penati  imeonekana kuwa na makosa mara baada ya video kurudiwa na kuonyesha mpira huo haukushikwa bali uligonga gotini kwa mchezaji huyo

                                             penati iliyopelekea lamptey kufungiwa

mara baada ya mtanange huo FIFA ilitoa tamko kurudiwa kwa mechi hiyo novemba 16 mwaka huu . huku ikisema refa joseph lamptey anafungiwa soka kwa kuvuruga mchezo huo.


             wachezaji wa Africa kusini wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 ambao umefutwa kwa sasa

Post a Comment

0 Comments