advertise with us

ADVERTISE HERE

EVERTON WAMTAKA CAVANI BAADA YA KUMKOSA DIEGO COSTA

Everton wanahaha kumtafuta mbadala wa Romelu Lukaku alietimkia Manchester United na  baada ya kumkosa Diego Costa alietimkia Atletico Madrid
 Taarifa za ndani zinadai mchezaji huyo kwa sasa hana furaha tangui kuwasili kwa Neymar katika timu hiyo na ameonyesha kutaka kuondoka.
Kocha wa Everton Ronald Koeman anajipanga kuongeza dau kumpata mshambuliaji huyo wa Uruguay na Paris-saint Germain.
Taarifa za ndani zinadai Koeman atakutana na uongozi wa PSG na kuzungumzia uhamisho wa mchezaji  huyo anaeonekana kufaa kuziba nafasi ya Lukaku.

Mara ya kwanza Everton ilitoa ofa kwa Diego Costa akiwa chelsea lakini mchezaji huyo aliikataa na kurudi Atletico Madrid.

Kwa upande wa PSG Cavani amehusishwa na kutaka kuondoka kutokana na uwepo wa Neymar Jr aliesajiliwa msimu huu kwa Euro milioni 200 na utofauti wao ulianza kkatika mechi dhidi ya Lyon  baada ya kugombania penati aliyokosa.
kuna uvumi  umesambazwa kuhusu  Cavani kupewa kiasi cha  euro 880,000 ali amwachie Neymar jukumu la kupiga penati katika timu hiyo, "PSG inakataa taarifa za uongo zilizosambaa mitandaoni kumpa fedha  Cavani asipige penati na  Neymar pekee ndio ahusike na jukumu hilo " kilisema chanzo hicho

Post a Comment

0 Comments