advertise with us

ADVERTISE HERE

DIEGO COSTA KUTIMKIA AL HILAL

Diego Costa kukipiga kwa mkopo katika klabu ya Al Hilal baada ya kujiunga na klabu ya Atletico Madrid akitokea Chelsea kwa dau la paundi milioni 53.

Diego Costa  ameonekana katika mji mkuu wa hispania na maskani ya klabu yake ya zamani Atletico Madrid, alionekana akiwa na jezi ya timu hiyo akifuatilia mechi ya Atletico Madrid dhidi ya As Roma

 Diego costa atakipiga katika kwa mkopo  klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia endapo dili la  kujiunga Atletico Madrid litafanikiwa.Costa alirejea Atletico Madrid na kuilazimisha klabu hiyo imsajili.

Costa alitua jijini madrid akitokea Brazil alikokuwa mapumzikoni, pia costa alizungumza na uongozi wa Chelsea na kuwaeleza hato rejea Darajani mpaka atakapokamilisha kujiunga na Atletico Madrid.

Costa hajashiriki mazoezi na klabu ya chelsea Tangu alipoambiwa hayumo kwenye mipango na kocha wa timu hiyo Anton conte pia ni juzi tu Gari ya Diego costa iliondolewa kwenye paki ya wachezaji kikosi cha kwanza .

Costa alijiunga na chelsea akitokea Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 32 akicheza michezo 109 na kufunga magoli 58 na atarejea Atletico madrid kwa dau la paundi milioni 53.
 


Post a Comment

0 Comments